February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

HAITI YAOMBA MSAADA WA KIJESHI

Serikali Haiti imeomba kutumiwa vikosi vya kigeni kutumwa nchini humo ili kulinda miundo mbinu muhimu baada ya Rais wa Taifa hilo,Jovenel Moise kuuwawa juma lililopita.

Haiti imetuma ombi hilo kwa serikali ya marekani na Umoja wa Mataifa.Hata hivy Marekani imesema imetupilia mbali ombi ombi hilo na kueleza kuwa haina mpango wa kutuma wanajeshi wake na mbadala wake watatuma maafisa wa FBI kusaidia katika uchunguzi.

Mauaji ya Rais huyo yakitokea siku ya Jumatano juma lililopina na washukiwa 17 wa mauaji hayo walikamatwa wakiwemo wanajeshi wastaafu kutoka nchini Colombia huku Washukiwa wengine watatu waliuawa na wengine wanane, bado wanatafutwa.