February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

GHANA: MKE WA RAIS KURUDISHA FEDHA ZA MARUPURUPU ALIZOLIPWA

Rais wa Ghana akiwa na mkewe

Mke wa rais wa Ghana,Rebecca Akufo-Addo amesema anarejesha fedha zote za marupurupu anayolipwa tangu Rais aingie madarakani mwaka 2017 baada ya wananchi wa taifa hilo kulalamikia kuhusu mshahara huo anaolipwa.

Katika taarifa aliyoitoa First Lady huyo amesema kuwa atarudisha fedha zote kiasi cha Dola za kimarekani 151,618 sawa na  shilingi Milioni 348 za Kitanzania kwani hakuomba kulipwa na anapokea fedha hizo kutokana na wadhifa alionao kama mke wa Rais ingawa si malipo rasmi.

Ameongeza kuwa amefikia uamuzi wa  kurudisha fedha hizo kutokana na maoni mabaya yaliyotolewa  na baadhi ya wananchi yakidai kuwa fisadi, mbinafsi na mwanamke asiyejali maslahi ya watu wa taifa hilo.

Nchini Ghana Mke wa Rais na mke wa makamu wa Rais wanapokea marupurupu kutokana na nyadhifa hizo na Bunge la nchi hiyo limethibitisha malipo ya wake hao kuwa kiasi cha Dola 3,500 kila mwezi sawa na Shilingi za Kitanzania Milioni nane kiwango sawa na wanacholipwa mawazir suala ambalo limepingwa vikali na wananchi wa taifa hilo.