February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

GAZETI LA UHURU LAPIGWA KUSHOTO NA KULIA

Na Leonard Mapuli


Serikali imetangaza kusitisha kwa siku 14 leseni ya uchapishaji wa gazeti la kila siku la Uhuru,linalomilikiwa na Chama cha Mapinduzi CCM,baada ya kuchapisha taarifa ya uongo katika ukurasa wake wa mbele leo Agosti11, kuwa Rais Samia amesema hatowania urais mwaka 2025.


Hatua hii ya serikali imekuja saa mbili tu baada Chama cha Mapinduzi ambao ni wamiliki wa gazeti hilo,na kwakuzingatia kuwa aliyeandikwa kwa taarifa zisizo za ukweli ni M/kiti wa Chama taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano kuishauri bodi ya Kampuni kukutana kwa dharura,na baada ya kukutana,bodi hiyo ilikubaliana kusitisha uzalishaji wa gazeti hilo na kuwasimamisha vigogo watatu ambao ni Mkrugenzi Mtendaji Ernest Sungura,Mhariri mtendaji Athuman Mbutuka,na Msimamizi wa gazeti hilo Rashid Zahoro.


“Hawa walionekana kuhusika moja kwa kwa moja kwenye usimamizi,na ninaipongeza bodi kwa hatua waliyochukuwa kwani uko ndani ya mamlaka yao”,amesema Daniel Chongolo,katibu Mkuu wa CCM.

Gerson Msigwa-Mkurugenzi,Habari (MAELEZO)


Taarifa iliyosababisha madhira yote haya,ilichapishwa ukurasa wa mbele kama “Habari uza” katika gazeti hilo kwa siku ya Jumatano,Agosti 11 na kunukuu maneno ambayo Rais Samia hakuyazungumza wakati wa Mahojiano yake na shirika la Utangazaji la Uingeleza BBC,Agosti 9 mwaka huu.


“Tunamuomba sana Rais radhi,kwa kumlisha maneno”,ameongeza Chongolo.


Kwa mujibu wa barua ya serikali na taarifa kwa umma juu ya kusitishwa leseni ya uzalishaji kwa majuma mawili,Mkurugenzi wa Idara ya Habari(MAELEZO),Gerson Msigwa,ameutaka uongozi na wamiliki wa gazeti hilo kufuata sheria endapo hawajaridhika na uamuzi wa serikali,na wanaruhusiwa kukata rufaa.