February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

FOLENI NDEFU YA MAGARI KIBAHA YAZIDI KUTISHA.

Baadhi ya wasafiri wanaotumia barabara Kuu ya Dar es Salaam kuelekea  Morogoro na mikoa mingine wamelalamikia uwepo wa foleni kubwa ya magari kila siku katika maeneo yanayoanzia Kibaha Picha ya ndege, Kongowe na Kwa Mathias mkoani Pwani inayoleta usumbufu mkubwa.

Watetezi Tv imefika katika eneo la Kibaha na kushuhudia na msururu mrefu wa magari ya abiria na mizigo yakisubiria kupungua kwa foleni ya iliyochukua zaidi ya saa matatu kabla ya magari kuanza kuondoka katika eneo linaloanzia Kibaha Picha ya ndege, Kwa Mathias, Kongowe hadi Mlandizi.

Baadhi ya abiria na madereva wamelalamika kuwa foleni hiyo licha ya kuleta usumbufu mkubwa kwa abiria na watumiaji wengine wa barabara imekuwa chanzo cha kuibuka kwa vitendo vya uhalifu hasa wizi.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo amekiri kuwepo kwa tatizo hilo na kudai kuwa limesababishwa na adha ya mvua iliyoharibu barabara ya mchepuko kupisha upanuzi wa barabara katika eneo hilo.

“Mkandarasi alijenga barabara ya mchepuko kwa kutumia katika eneo la barabara ya zamani lakini kutokana mvua,malori ya mizigo yameiharibu”,amesema Mhandisi Ndikilo.

Ni takribani majuma mawili sasa tangu kuwepo kwa foleni kubwa ya magari isiyo ya kawaida katika eneo la Kibaha mkoani Pwani  inayotokana na barabara ndogo iliyopo hivi sasa kuelemewa na idadi kubwa ya magari kufuatia ujenzi wa kupanua barabara hiyo unaoendelea hivi baada ya Mvua kuharibu barabara iliyokuwa ikitumika kwa muda.