February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

FISI AVAMIA MAKAZI YA WATU NA KUZUA TAHARUKI

Na Rodrick Mushi, Kilimanjaro

Fisi ameibua taharuki kwa wakazi wa Kijiji cha Kwa Sadala Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro baada ya kuvamia makazi ya watu katika Kitongoji cha Dipu na kuua kondoo saba.

Adam Alex mkazi wa Sadala na ambae pia mifugo yake iliuliwa na fisi huyo ameeleza kuwa fisi huyo aliingia  kwenye makazi yao May 20 majira ya usiku na kuingia kwenye nyumba kadhaa za wakazi wa eneo hilo na kuua mifugo.

Diwani wa Kata ya Masama Kusini Cedrick Pangani amekwishafika katika eneo la tukio na kuthibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akiwapa pole wanachi waliopoteza mifugo yao na kueleza kuwa tayari mamlaka ya maliasili na utalii imekwishafika Kijijini hapo na kuanza kufanya juhudi za kumsaka fisi huyo ili kuepusha madhara zaidi.