February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

FANYENI HARAKATI CHANYA, IBUENI MAOVU YANAYOFANYIKA – RAIS SAMIA

Rais Samia amesema kuwa katika serikali yake hakuna mapambano bali kuna sera za upatanisho, maridhiano na kuwaunganisha Watanzania pamoja, amesisitiza kuwa hakatazi uhanarakati chanya na kuibua maovu mbalimbali yanayofanyika.
“Uanaharakati unaweza kuwa vyote, siwakatazi kuwa wanaharakati mnaweza kuwa chanya na au hasi lakini uanaharakati chanya unajenga Zaidi. Fanyeni uanaharakati ibueni maovu yanayofanyika. Njooni tukae tuzungumze,” amesema rais Samia.
Amewataka wadau hao kupeleka malalamiko yao serikalini ili yafanyiwe kazi, ameeleza kuwa aliviambaia vyama vya siasa kuwa hakuna haja ya kuwa na mapambano kwa kuwa wote ni watanzania na kuwasihi kama kuna changamoto ni muhimu kukaa kwa pamoja kutafuta suluhu kwa mazungumzo kuliko kujigawa mafungu.
“Hapa wote ni Watanzania hakuna wa kwenda kupambana na Serikali. Unapambana na Serikali kwa jambo gani? Niliwaambia wenzetu wa vyama tunapambana kwa kitu gani wote tunaendesha siasa za Tanzania, lengo letu kuijenga Tanzania,” amesema Rais Samia.
“mnajigawa mafungu mnakwenda mnapambana, mnapambana kwa jambo gani? Ndiyo maana tukasema fanyeni harakati za haki za binadamu kulingana na mazingira ya kitanzania, kama mliokuwa wanaharakati wa ‘aluta continua’ badilikeni wanangu.”ameae Rais Samia Suluhu Hassan