February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

FAMILIA YA PADRI KANGWA YASEMA IMEPOKEA KIFO CHAKE KUWA NI BARAKA

Familia  ya aliyekuwa Mkuu wa Wamisionari Afrika nchini Tanzania, Padri Francis Kangwa, imesema imepokea kifo cha ndugu yao kama baraka na wanasherehekea maisha yake ulimwenguni wakati alipokuwa hai.Hayo yamesemwa hii leo wakati wa misa ya mazishi ya Padri Kangwa yanayofanyika katika Kituo cha Hija kilichopo Pugu mkoani Dar es salaam.

“Hatutaki kubishana na Mungu, tumepokea kifo chake. Huu ni ujumbe kwa ulimwengu kwamba kifo cha Padri Kangwa ni baraka na tutasherehekea maisha yake,” amesema William,kaka wa Marehemu Francis Kangwa

“Ujumbe wa Familia ya Kangwa ni kwamba tumepokea kifo cha Father Francis, hatujali vipi, wapi, nani anajua, hatuhitaji kujua,” imesema familia hiyo.

“ujumbe wetu kwenu, tumepokea taarufa za  kuondoka kwa kaka yetu bila wakati, tumwfikiri bila wakati sababu ndiyo niia iliyohitimisha maisha yake. Tunamshukuru Mungu kwa muda aliompa wa kuwatumikia watu wake.”

Mwili wa Padri Kangwa, ulikutwa kwenye tanki la maji la nyumba ya mapadri iliyopo jengo la Ottoman jijini Dar es Salaam, siku ya tarehe 15 Aprili,2022.