February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

“FAHAMUNI DHAMANA YA MAJUKUMU MLIYOBEBA” RAIS SAMIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan hii leo amewaapisha wakuu wa mikoa Pamoja na wakuu wa taasisi mbali mbali akiwemo mkurugenzi mkuu wa Tasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU, Pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa mashtaka wa Serikali DPP Pamoja na wasaidizi wao.

Akizungumza na jopo la viongozi waliohudhuria sherehe hizo Rais Samia amewapongeza wakuu wa mikoa walioteuliwa kushika nafasi hizo na kuwataka kufahamu dhamana ya majuku waliyobeba na kusimama na Mungu katika majukumu hayo waliyopatiwa.

Kwa upande wake Makamu wa Rais Dkt. Phillip Mpango Amezungumza na jopo la viongozi waliohudhuria sherehe za kuapishwa kwa viongozi hao Ikulu jijini Dar es Salaam, na kuwasisitiza vongozi walioapishwa leo kuzingatia sifa za viongozi kuwa Hodari wa kazi Pamoja na kuwa mfano kwa tabia njema.

hatutarajii viongozi waliopewa dhamana na kuapishwa leo kuwa na tabia zisizofaa, sitarajii kwamba kutakuwa na walevi kati yenu, sitarajii kuwa na orodha ya wazinzi ambao wanafika katika ngazi zetu na mengine maovu katika jamii yetu”

Dkt. Mpango

Dkt Mpango ameongeza kuwa, Moja ya majukumu ya viongozi na hasa wakuu wa mikoa ukiacha ulinzi na usalama ni kusimamia uchumi wa mkoa pia amewataka viongozi hao kusimamia ipasavyo chumi za mikoa kwa umakini Zaidi huku wakijielekeza kuongeza uzalishaji na hasa kwenye kilimo Pamoja na viwanda.

Lakini pia msimamie tija, muangalie masoko ya wananchi na hasa wakulima wetu, na huko ndipo tutakapopata Maisha bora Zaidi kwa wananchi wetu ambao wanahangaika kila siku

Ameongeza  Dkt Mpango

Pia Dkt Mpango amewataka wakuu wa mikoa kutoonea watu wakati wa utekelezaji wa majukumu yao.

Mkashughulike na wazembe, na wabadhilifu na wale wasio na nidhamu, angalizo langu ni moja tu, msitumie madaraka yenu vibaya mliyokabidhiwa kwa heshima kabisa na Rais, msionee watu na mkatende haki”

Dkt. Phillip Isdory Mpango, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Kwa Upande wake waziri mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa Majaliwa amewataka wakuu wa mikoa kutambua majukumu yao na kujifunza kujua mahitaji ya taasisi zao.

Jambo muhimu ni kutambua majukumu ya nafasi uliyopewa kwenye eneo lako, kama ni mkuu wa mkoa jua majukumu yako, kama ni mkuu wa taasisi jua majukumu yako,  na jifunze nini kinatakiwa kwenye taasisi yako, mipaka yake, wasaidizi wako ili uweze kufanya kazi yako vizuri Zaidi.

Kassim Majaliwa

Hata hivyo Rais Samia amefanya mabadiliko kwa wakuu wa mikoa wawili David Kafulila aliyeteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Arusha, Pamoja na John Mongela aliyeteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Simiyu, katika mabadiliko hayo John Mongela amehamishiwa Arusha badala ya Simiyu, huku Kafulika akipelekwa Simiyu badala ya Arusha.