February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

ETHIOPIA : MFUNGWA AMEZA MISUMARI 30

Mkuu wa Hospitali ya Arbaminch nchini Ethiopia amesema wameondoa misumari 30,chuma na vitu vingine katika tumbo la mfungwa mmoja nchini humo.Mfungwa huyo ambaye ana matatizo ya akili anakabiliwa na kifungo cha miaka saba jela.

Mfungwa huyo alilazwa katika hospitali hiyo Jumanne iliyopita baada ya kupata maumivu ya tumbo na hali yake kuwa mbaya na alipoulizwa na madaktari alisema amemeza misumari.

Baada ya kupiga picha ya X-ray madaktari waligundua kuwepo kwa misumari na vipande vya chuma tumboni na mfungwa huyo alifanyiwa upasuaji.

Mdaktari hao walitoa takriban misumari 30, kalamu nne, sindano, uzi na vipande vya chuma katika tumbo la mfungwa huyo. Baada ya upasuaji, madaktari walipiga picha ya x-ray ya mtu ili kuthibitisha kama hakuna kitu kingine kilichoachwa ndani ya tumbo lake na kwasasa inaelezwa yupo katika hali nzuri hata hivyo anatahitaji uchunguzi wa katika koo lake.

Chanzo : BBC Swahili