March 23, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

ETHIOPIA: AJIUNGA CHUO KIKUU AKIWA NA MIAKA 69

Raia mmoja wa Ethiopia,Tadesse Ghichile (69) amejiunga na Chuo Kikuu cha Jimma ambako anatarajiwa kuhitimu shahada ya Matibabu.

Ghichile ni baba wa watoto 11,ni mkulima na pia anauza mgahawa kijijini kwake ili aweze kuitunza familia yake.Akiwa yatima katika umri mdogo aliacha shule akiwa darasa la nane.

Takribani miaka 10 iliyopita Ghichile alichukua uamuzi wa kurudi katika mfumo rasmi wa elimu na kufaulu mtihani wa kitaifa wa kuingia chuo kikuu.

Anasema Kwa muda mrefu alikuwa amepata ugumu kurudi shuleni baada ya kuanzisha familia. Lakini alidhamiria kumaliza hadi mwisho.