Na Leonard Mapuli (lennymapuli@gmail.com)
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam,leo Agosti 6,imesoma shauri la kesi namba 63vya mwaka 2020 inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia (CHADEMA),Freeman Mbowe. Na wenzake watatu.
Katika kesi hiyo iliyokwama kusikilizwa jana (Agosti 5) mawakili wa upande wa serikali waliiomba Mahakama hiyo kusoma upya mashtaka yanayowakabili watuhumiwa hao wanne,kutokana na kwamba,watatu kati yao,hawakuwepo mahakamani hapo wakati kesi hiyo ilipotajwa kwa mara kwanza Julai 26 mwaka huu bila uwepo wa washtakiwa namba 1,2,na 3 wa kesi hiyo.
Baada ya kusomwa kwa kesi hiyo,mawakili wa serikali wakiongozwa na wakili mwandamizi Pius Hilla wameiambia mahakama kuwa uchunguzi wa kesi hiyo bado haujakamilika na hivyo kuiomba Mahakama kupanga siku nyingine ya kusikiliza tena kesi hiyo.

Hata hivyo,hakimu anayesikiliza kesi hiyo,Thomas Simba ameshangazwa na upande wa ofisi ya mkurugenzi wa Mashtaka ambayo kwa mujibu wa mashtaka yaliyowasilishwa na ofisi hiyo mahakamani hapo Julai 26,yalieleza kuwa uchunguzi ulikuwa umekamilika,lakini leo ofisi hiyo hiyo inasema uchunguzi haujakamilika.
“Tumeshakamilisha uchunguzi,tatizo ni jalada la kesi hii kuwa bado lipo katika ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka,ni kwamba tu taarifa bado hazijaandaandaliwa kwa ajili ya kupelekwa kwenye mahakama kuu”,amejibu wakili wa serikali,Pius Hilla mahakamani hapo.
Kwa mujibu ya sheria,Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu haina Mamlaka ya kusikiliza kesi ya jinai inayomkabili Mbowe na wenzake kutokana na mipaka ya kimahakama,na kesi hiyo inapaswa kusikilizwa katika Mahakama kuu ya Tanzania imbayo ndiyo yenye Mamlaka kisheria.

Wakili Peter Kibatala,akiwa miongoni mwa mawakili tisa wanaomtetea Mbowe na wenzake,amesema kitendo cha upande wa mashtaka kuwasilisha taarifa mbili tofauti,juu ya kukamilika na kutokamilika kwa uchunguzi,inazidi kuongeza utata na kuipaka matope mahakama.Kibatala ameimba mahakama hiyo kuutaka upande wa mashtaka kuheshimu mashtaka iliyowasilisha mahakamani hapo Julai 26.
Baada ya kusikiliza pande zote mbili,Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu imepanga kusikiliza tena kesi hiyo Ijumaa ijayo,Agosti 13 ili iweze kupeleka shauri hilo katika Mahakama Kuu kwa hatua za juu zaidi za usikilizwaji wa kesi hiyo.

KUWASILI KWA MBOWE MAHAKAMANI
Mapema asubuhi ya leo (Agosti 6),idadi kubwa ya askari polisi wa kutuliza ghasia,wenye silaha mbalimbali,walitanda katika barabara zote zinazotumiwa na watu Pamoja na vyombo vya usafiri kufika mahakamai hapo,huku pia kukiwa na idadi kubwa ya magari ya polisi ya wazi,pamoja na gari maalumu lenye maji ya kuwasha maarufu ‘Washawasha’.Watu wote walioingia mahakamani hapo walipekuliwa na kuombwa vitambulisho huku baadhi wakizuiliwa kuingia mahakaani hapo.

Mbowe na wenzake,waliwasili mahakamani hapo majira ya saa mbili asubuhi,akiwa amepakiwa kwenye basi la Magereza lililosindikizwa na magari madogo matatu yenye askari wenye silaha .
VUTA NIKUVUTE NJE YA MAHAKAMA
Wakati kesi ikiendelea ndani ya mahakama,baadhi ya viongozi wa CHADEMA waliofika mahali hapo wakiwemo waliowahi kuwa wabunge,walizuiliwa kuingia ndani ya mahakama.Taarifa Zaidi zimeeleza kuwa baadhi wamevutana na polisi hadi kukamatwa na kupelekwa kiktuo kikuu cha polisi kati.

Katika hatua nyingine,Polisi walijikuta katika Vuta ni kuvute nyingine na jopo la mawakili wa Mbowe,ambapo Peter Kibatala (Wakili) alizuiwa kwa muda na maafisa wa polisi kuzungumza na wandishi wa Habari waliokuwa wamefurika mahakamani hapo.Kibatala alikuwa akiwapa wandishi mrejesho wa kilichotokea mahakamani na tafsiri za sheriakwani wandishi hawakuruhusiwa kusikiliza kesi hiyo ndani ya mahakama na hivyo kubaki nje ya ukumbi wa Mahakama.Mvutano wa Kibapata na polisi ulidumu kwa mud ana kutunishiana misuli.
“Mahakama siyo mali yako”,alisikika Kibatala akimwambia kiongozi wa polisi waliokuwa wakishika doria mahakamani hapo.Hata hivyo baadae Polisi walimruhusu Kibatala kuzungumza na wandishi baada ya makubaliano na Polisi.
UPINZANI.
Zitto Kabwe,Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo na James Mbatia,M/kiti wa Chama cha NCCR Mageuzi,ni viongozi wakuu wakuu wa vyama vya siasa waliofika mahakamani hapo hapo kufuatilia kesi hiyo ambapo wote wawili wameahidi kutoa mawakili toka kwenye vyama vyao,kuungana na mawakili wanaomtetea Freeman Mbowe na wenzake.
Katika kesi hii,Freeman Mbowe na wenzake ambao ni Halfan Bwire,Adam Hassan,na Mohamed Lingwenya, wanakabiliwa na makosa ya kupanga njama za kulipua vituo vya mafuta,pamoja na mikusanyiko kinyume na vifungu namba 4 (1),3 (i),na 27 (c) vya sheria namba 21 ya mwaka 2002 ya kuzuia ugaidi,na kufadhili ugaidi,kinyume na sheria ya kuzuia ugaidi yam mwaka 2002.
Watuhumiwa watatu (Ukimtoa Mbowe),wamesota rumande tangu Agosti 19 mwaka 2020,kabla ya Mbowe kuunganishwa kwenye kesi hiyo Julai 20,baadaya kumatwa Pamoja na viongozi wengine 10 wa CHADEMA wakiwa jijini Mwanza usiku wa manane,saa chache kabla ya kufanyika kwa Kongamano la Katiba Mpya.
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),kinahusisha kukamatwa kwa mwenyekiti wake kutokana nay eye kuwa mstari wa mbele kuhamasisha vuguvugu la katiba Mpya nchini Tanzania.
Habari Zaidi
BULAYA AHOFIA MUSTAKABALI WA WANAHABARI SAMIA AKIONDOKA MADARAKANI
THRDC YAKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA UBALOZI WA JAPAN
THRDC YAWAJENGEA UWEZO WANACHAMA WAPYA WA MTANDAO