February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

DPP AFUTA KESI INAYOWAKABILI KINA MBOWE

Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), Sylvester Mwakitalu, amewasilisha hati ya kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi yenye mashitaka ya ugaidi  inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu.

Mwakitalu amewasilisha ombi hilo hii leo katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Rushwa na Ujumumu Uchumi jijini Dar es salaam mbele ya Jaji Joachim Tiganga ambapo Mbowe na wenzake walitarajiwa kuanza kutoa utetezi wao hii leo.

Wakili wa Serikali,Robart Kidando amemueleza Jaji kwa wana ombi moja la kufanya mbele ya mahakama yako, na ombi hilo ni kuhusu mkurugenzi wa mashtaka kwa niaba ya Jamhuri ameomba kuwasilisha taarifa ya kutokuwa na nia ya kuendelea zaidi na shauri hilio na taarifa hiyo wameitoa chini ya kifungu cha 91 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai.

“Tunaomba kuondoa mashtaka yote dhidi ya washtakiwa wote na kuiondoa kesi hiyo ambayo tumeiwasilisha mahakamani.”

Jopo la Mawakili wa Utetezi wakiongozwa na Peter Kibatala hawakuwa na pingamizi juu ya ombi hilo na kuiachia mahakama.