February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

DKT MWINYI KUHUDHURIA MKUTANO WA DHARURA SADC,AFANYA PIA UTEUZI MZITO Z’BAR.

Dkt.Hussein Mwinyi-Rais wa Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi anatarajia kushiriki katika Mkutano wa dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali (SADC Extraordinary Double Troika Summit) unaojumuisha Nchi wanachama ambazo ni Msumbiji (Mwenyekiti wa SADC),Malawi, Tanzania,Botswana,Afrika Kusini na Zimbabwe.

Mkutano huo utafanyika katika mji mkuu wa Msumbiji,Maputo kesho (Alhamisi) Mei 27.

Katika taarifa aliyoitoa kupitia ukurasa wake rasmi katika mtandao wa Twitter,Rais Mwinyi hajaweka bayana endapo anahudhuria mkutano huo kumuwakilisha Rais  wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Samia Suluhu ama yeye kama rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Katika Hatua nyingine,Rais Dkt Mwinyi amemteua Dkt Ali Ahmed Uki kuwa Mkuu wa Skuli ya Shera ya Zanzibar ( The Law School of Zanzibar).Uteuzi huo unaanza Mei 26,mwaka 2021.