March 23, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

DKT. GWAJIMA AFUNGUKA, ATAKA VIONGOZI KUTOLETA MZAA KUIKABILI CORONA

Na Antonio Benedicto

Tayari Tanzania imeripotiwa kuwa na visa zaidi ya 800 vya wagonjwa wenye maabukizi ya Corona na vifo 29, Waziri mwenye wa afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Dorothy Gwajima amewataka vingozi kusimamia mapambano ya janga hilo na kuwa wakishindwa kufanya hivyo Serikali haitawavumilia.

“Napenda kuweka wazi kuwa, serikali haitaendelea kuvumilia kuona baadhi ya viongozi hawatimizi wajibu wao kwenye kusimamia mapambano dhidi ya UVIKO-19 ” amesema Waziri wa Mendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Dorothy Gwajima.

Pia Waziri, Dorothy Gwajima amesema Serikali inafatilia kwa ukaribu maelekezo yote yanayoelekezwa kutekeleza na edapo itaona ulegevu kwa baadhi ya viongozi katika utekelezaji huo hatua za zitachukuliwa kwao kwa kuzingatia sheria na taratibu.

Serikali ya Tanzania tayari imeripoti kuanza kutoa chanjo za Corona, huku hospital za kanda Bugando iliyoko Mkoa wa Mwanza na KCM ya Mkoani Kilimanjaro kwa mara tofauti zimeripoti kuwa na uhaba wa mitungi ya gesi kwa wahanga wenye matatizo ya upumuaji ambayo yanatajawa kuwa ni dalili mojawapo ya UVIKO-19.