March 23, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

DCI KINGAI ASISITIZA WAZAZI KUZINGATIA MALEZI BORA KWA WATOTO WAO ILI KUPUNGUZA UKATILI

Mkurugezi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), ACP. Ramadhan Kingai amewahasa wazazi kuzingatia umuhimu malezi bora kwa watoto wao hususani wa kike, ambapo amedai kuwa kufanya hivyo kutapunguza matukio ya ukatili amabayo yamekuwa yaliripotiwa Nchini.
Akizungumza washiriki wakati wa kufunga mafunzo yaliyoandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu kwa kushirikiana na Shirika la C-SEMA kwa maofisa wa Jeshi la Polisi pamoja na Wanasheria kutoka Ofisi ya Taifa ya mashtaka yakijadili masuala ya ukatili wa kijinsia na unayanyasaji wa watoto amesema kuwa watoto kukosa malezi yanayostahiki imekuwa kati ya vyanzo ambavyo vimekuwa vikipelekea ukatili wa kijinsia.
Ametolea mfano tukio ambalo amesema limetokea mkoani Mtwara kuwa mtoto (15) aliuawa lakini akidai kuwa mazingira yaliyopelekea mauaji yalipelekewa na kukosa malezi stahiki, hali ambayo ilipelekea mtoto huyo kuingiwa na tamaa.
“Kuna kesi moja mtoto wa miaka 15 ameuawa lakini sababu ni kwamba ameweka foleni ya wanaume amechukua pesa zao lakini hajawatimizia kama walivyokuwa wanataka lakini ukiangalia sababu nyuma yake huyo msichana aliachiwa watoto wawili Mama yake hata hajulikani yuko wapi” amesema DCI, ACP Ramadhan Kingai
Aidha (DCI) Ramadhan Kingai amewataka maofisa wa upelelezi kwenye Mikoa kufuatilia kwa ukaribu kesi za ukatili wa kijinsia pamoja na unayanyasaji wa watoto, lakini lakini ameshauri madawati hayo kupangiwa maofisa ambao wataweza kufanya kazi kwa ubora ili kutokomeza matukio ya ukatili.