February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

DCI KENYA ATUPWA GEREZANI KWA KUIDHARAU MAHAKAMA

Mkurugenzi wa Upelelezi wa makosa ya jinai nchini Kenya,George Kinoti amehukumiwa kifungo cha miezi minne jela baada ya kuidhrau mahakama baada ya kushindwa kutii amri ya mahakama iliyomtaka kurudisha bunduki alizompokonya mfanyabiashara anayetazamiwa kuwania kiti cha urasi nchini humo 2022,Jimmy Wanjigi mwaka 2017.


Kinoti anatazamiwa kujisalimisha katika gereza la Kamiti ambalo linatajwa kuwa na ulinzi mkali siku saba tangu hukumu hiyo itolewe na akishindwa kufanya hivyo DPP ameagizwa kutoa hati ya ukamataji dhidi yake.


Mnamo mwezi Juni mwaka 2019, Jaji Chacha Mwita wa Mahakama Kuu ya Nairobi alitoa uamuzi kwaba serikali haikutumia busara kwa kuchukua bunduki hiyo ilhali bado mmiliki alikuwa na leseni halali ya umiliki na kueleza haki za Wanjigi zilikiukwa na kitendo hicho kilitawaliwa na nia ovu.


Mahakama hiyo pia ilitoa siku 30 kwa DCI Kamiti kurudisha silaha hiyo kwa mmiliki wake na ukomo wa agizo hilo ilikuwa tarehe 25 Machi, 2021 hata hivyo alishindwa kutii agizo hilo hivyo Wanjigi alifungua kesi na kuitaka mahakama iwatie hatiani kwa kuidharau mahakama.