February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

DAKTARI ALIYEMTIBU MKOSOAJI WA VLADMIR PUTIN ATOWEKA

Jeshi la Polisi nchini Urusi limesema kuwa Daktari aliyekuwa akimhudumia mwanasiasa wa upinzani na mkosoaji mkubwa wa Rais Vladmir Putin,Alexei Navalny ametoweka baada ya kupteza fahamu kwenye ndege inayofanya safari zake nchini Urusi na mpaka sasa hajulikani alipo
Daktari huyo Alexander Murakhovsky anadaiwa kuwa aliondoka kwa gari kutoka katika eneo moja siku ya Ijumaa na hajaonekana tena tangu wakati huo, hata hivyo juhudi za kumtafuta kwa kutumia ndege zisizo na rubani, helikopta na askari wa ardhini linaendelea.
Dkt Alexander Murakhovsky alikuwa mkuu wa huduma za kitabibu katika hospitali ya Omsk wakati Navalny alipolazwa huko baada ya kupewa sumu na siku chache baadae daktari huyo alipandishwa cheo na kuwa Waziri wa Afya katika mkoa wa Omsk.