February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

“CORONA IPO,CHUKUENI TAHADHARI”

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,Prof Abdiel Makubi amesema vifo vinavyotokana na ugonjwa wa corona vipo ingawa si kwa kiwango kikubwa na kuongeza kuwa baadhi ya mikoa kuna maambukizi ya covid-19 na kuwataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari.


“Nawasisitiza wananchi kuendelea kujikinga na corona na kuendelea kunawa mikono kwa maji safi tiririka au vipukusi (sanitizer),kufanya mazoezi,kula lishe bora bila kusahau tiba asili,”ameeleza Prof.Makubi


Aidha ameongeza kuwa wameweka utaratibu katika viwanja vya ndege na mipakani wa kupima wageni wanaowasili nchini kupimwa corona kwa lazima ili kudhibiti na kuzuia maambukizi ya virusi vipya vya corona vinayoibuka.