March 23, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

COASTER ILIYOUA MORO ILIBEBA MASHADA YA MAUA BILA MAITI:DEREVA ALIDANGANYA ASKARI KUWA ANAWAHI KUZIKA.

Dkt. Kess Ngarawa-Kaimu Mganga Mfawidhi-Morogoro

Idadi ya watu waliopoteza maisha katika ajali iliyohusisha magari matatu mkoani imeongezeka na kufikia 9.Kwa mujibu wa Kaimu mganga mfawidhi wa katika hospitali ya  Rufaa ya Morogoro Dkt Kessy Ngarawa ,idadi ya miili iliyofikishwa hospitalini hapo jana usiku ilikuwa ni 7 na kwamba vifo vingine vilitokea majeruhi wakiwa wameshafikishwa hospitalini hapo.

Taarifa kutoka hospitalini hapo pia zinaeleza  kuwa majeruhi waliofikishwa hospitalini hapo tangu jana walikuwa 25 na sasa wamebaki 23,kati yao watatu wako katika kuangalizi maalumu.

Baadhi ya majeruhi wanaopatiwa matibabu hospitali ya rufaa Morogoro.

Katika hali ya kushangaza,moja ya abiria waliokuwa katika basi dogo linalodaiwa kusababisha ajali hiyo amesema  gari hilo lilikuwa katika mwendo mkali na kila liliposimamishwa na askari wa usalama barabarani abilia walidai wapo safari moja wanakwenda kuzika huku gari hilo likiwa na mashada ya maua kuashiria kuwa kulikuwa mwili wa mtu aliyekuwa akisafirishwa lakini kwa mujibu wa abiria huyo gari halikuwa na maiti bali janja janja ya dereva kuhalalisha mwendo kasi.