Anthony Rwekaza
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Pwani kimelaani na kukemea tukio kukamatwa na kuendelea kuwashikiria wanachama wake wa BAWACHA kwenye kituo cha Mbweni jiji Dar es salaam na kulitaka Jeshi hilo kuwaachia bila masharti au kuwapeleka mhakamani.
Akizungumza na vyombo vya habari Jumatatu Oktoba 4, 2021, Afisa Habari Kanda ya Pwani Gerva Lyenda amesema askari Polisi waliwakamata wanachama hao ambao ni wanachama wa Baraza la Wanawake wa Chadema ( BAWACHA) siku ya Jumamosi Oktoba 2, 2021 walipofika kituoni kujua sababu ya kukamatwa kwa mwandishi wa Habari wa Mgawe TV Harlod Shemsunga ambaye amedai alikuwa anatekeleza majukumu yake ya kutafuta habari kwa kuwahoji makundi mbalimbali ya watu waliokuwa mazoezi (Jogging) wakiwemo wao kwenye viwanja vya Tanganyika Berkas.
Amesema Polisi walifika kwenye viwanja hivyo na kusitisha Jogging huku wakimkamata mwandishi huyo na kwenda naye kwenye kituo cha polisi Kawe, ambapo amedai wanachama hao sita waliambatana nao mpaka kituoni ili kujua sababu ya mwandishi huyo kukamatwa, amedai baada ya kufika nao walitiwa kizuizini na kuamishiwa kwenye kituo cha polisi Mbweni Jijini Dar es salaam , ambapo pia amedai walimshikiria mmiliki wa kituo cha Mgawe TV, Erenest Mgawe ambaye nae ameunganishwa na wenzake kwenye kituo cha Mbweni alipoenda kufuatiria kushikiriwa kwa Mwandishi wa kituo chake.
Pia Lyenda amesema wanachama hao wamegoma kula chakula wakiwa mahabusu ili kushinikiza kuachiwa bila masharti au kupelekwa Mahakamani ambapo amedai wameshikiriwa zaidi ya muda wa
masaa 48 unaolekezwa kisheria kukaa mahabusu.
Amedai chama hakitafanya utaratibu wowote wa kuwadhamini, hisipokuwa chama hicho kupitia wanasheria wake wameanza mchakato wa kuwasirisha barua maalumu Mahakamani ili iweze kutoa wito kwa Jeshi la Polisi kuwafikisha watu hao mbele ya Mahakama, huku akidai vitendo vya kuwakamata wafuasi wa Chadema vimekuwa endelevu, hivyo amelisihi Jeshi la Polisi kufuata sheria.
Ikumbukwe baada wanachama hao kukamatwa na taarifa kuanza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii,Jeshi la polisi kupitia Kamanda wa Jeshi hilo Kanda ya Dar es salaam, Jumanne Mliro alidai kuwa sabubu ya watu hao walikuwa na hisia zenye mitazamo wa kisiasa.

“Nimepokea taarifa ya watu waliokamatwa, walikuwa na viashiria vya uvunjifu wa amani kwa kutengeneza hisia zenye mtazamo wa kisiasa kupitia kivuli cha mazoezi,” alisema Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda ya Dar es salaam, Jumanne Muliro.
Vilevile Kamanda Muliro alidai kuwa wanaendelea uchunguzi kujilidhisha kama kubaini kama kulikuwepo na kusudi la uvunjifu wa amani kwenye sakata hilo, ambapo alidai kuwa baada ya kukamirisha uchunguzi taratibu nyingine za kisheria zitafuata.
Katika hatua nyingine Chadema kupitia msemaji wao wa Kanda ya Pwani wamelitaka pia Jeshi hilo kuwaachia bila masharti waandishi wa habari wanaodaiwa kushikiriwa kwenye vituo vya Polisi viwili tofauti akiwemo Mchora katuni, Optatus Fwema anayeshikiriwa kwenye kituo cha Polisi Ostarbay, Dar es salaam.
Wanachama hao wa Chadema wanaodaiwa kushikiliwa polisi tokea siku ya Jumamosi ni pamoja na Lilian Kimei, Rose Moshi, Hadja Mlolo, Rose Masiaka, Vailet David Seka, Leminda Rufyangira…
Habari Zaidi
BULAYA AHOFIA MUSTAKABALI WA WANAHABARI SAMIA AKIONDOKA MADARAKANI
THRDC YAKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA UBALOZI WA JAPAN
THRDC YAWAJENGEA UWEZO WANACHAMA WAPYA WA MTANDAO