March 23, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

CHADEMA WAMLILIA MBUNGE HAJI

Chama Cha Demokrasia Na Maendeleo (Chadema) Zanzibar kimeelezea kusikitishwa na Taarifa za kifo Cha Mbunge wa Konde, Khatib Hajji kwa tiketi ya Chama Cha ACT Wazalendo kilichotokea leo Mei 20, 2021 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Mbunge Khatib Hajji Akichangia hoja Bungeni enzi za uhai wake

Akizungumza Kwa niaba ya #CHADEMA Naibu Katibu Mkuu Chadema, Zanzibar Salum Mwalim ametoa pole kwa familia ya Marehemu, Kiongozi wa Chama Cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe, Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Zanzibar Nassor Mazrui, wananchi wa jimbo la Konde, Pamoja na Bunge kwa kumpoteza mbunge mahiri.

Marehemu ameacha alama ya harakati za mageuzi na kutetea haki na masilahi ya Zanzibar na Wa-Zanzibari, nakumbuka Bungeni mara ya mwisho Marehemu aliwazungumzia kwa kina Masheikh wa Uamsho wanaoshikiliwa kwa tuhuma za ugaidi akikumbushia madhila na kupatiwa haki zao.”

Salum Mwalimu, Naibu Katibu mkuu wa CHADEMA

Mbunge wa Jimbo la Konde kwa tiketi ya Chama Cha ACT Wazalendo Khatib Said Haji alipatwa na umauti katika Hospital ya rufaa ya Muhimbilii alipokuwa akipatiwa matibabu.