March 23, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

CHADEMA WALAANI VIKALI VITENDO VYA WANACHAMA WAO KUKAMATWA WAKIWA KWENYE MAENEO YA IBADA

Na: Anthony Rwekaza

Baraza la Wazee la Chama Cha Demokrasia na Mendeleo (CHADEMA), limelaani vikali vitendo vya wanachama wao waliovalia sare za Chama hicho kukamatwa na Jeshi la Polisi wakiwa kwenye maeneo ya ibada.

Akizungumza na vyombo vya habari kwa niaba ya wengine, Katibu Mkuu wa Baraza la Wazee wa chama hicho, Rodrick Lutembeka amelaani vitendo hivyo vya wanachama wa Chadema kushikiriwa na Jeshi la Polisi wakiwa kwenye shughli la kuambudu, amedai vitendo hivyo vinakiuka haki za Kikatiba na kuibua chuki na kuchochea uhasama kwa waumini.

“Vitendo vya ubaguzi na watu kukamatwa kanisani si tu vinakiuka haki za wakati kama zilivyoanishwa katika ibara ya 12&13 ya katiba bali vinaibua chuki kwa watu kuichukia serikali na kuchochea uhasama baina ya waumini wa dini” Katibu wa Baraza la Wazee wa CHADEMA, Rodrick Lutembeka

Pia kufuatia vitendo hivyo ambavyo Lutembeka amedai vimefanywa na Jeshi la Polisi amemtaka Rais Samia Suluhu Hassan wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ni Amri Jeshi Mkuu kukemea vitendo hivyo na Askali wanaohusika kuchukuliwa hatua ili kukomesha vitendo hivyo.

“Baraza la Wazee wa CHADEMA tunasema, askari wanaowakamata watu wanaokwenda kufanya ibada wanapaswa kuchukuliwa hatua kali na Amiri Jeshi Mkuu ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Samia Suluhu Hassan ili kuzima tabia hii ambayo inaonekana kuota mizizi” amesema Katibu Mkuu Baraza la Wazee CHADEMA, Rodrick Lutembeka

Aidha ametoa wito kwa mamlaka zilizowashikiria kuwaachia huru bila masharti wanachama hao wanaodaiwa kushikiriwa mpaka sasa, tokea siku ya Jumapili tarehe 15, Augosti 2021, Mkoani Mwanza, vilevile amewaomba wananchi kwaombea hili wandelee kupinga vitendo vya ukandamizaji, uonevu dhuluma na ubaguzi.

“Baraza la Wazee wa Chadema, tunataka serikali kuwakamata wafuasi wetu wa CHADEMA waliokamatwa huko Mwanza bila ya masharti yoyote. Na pia tunawaomba Watanzania watuombee ill Mungu atupe ujasiri wa kukataa vitendo vya ukandamizaji, uonevu, dhuluma na ubaguzi ” amesema Katibu Mkuu Baraza la Wazee CHADEMA, Rodrick Lutembeka