February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

CHADEMA WADAI RAIS SAMIA AMEIGILIA UHURU WA MAHAKAMA KUZUNGUMZIA SHAURI LA MBOWE

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan

Na: Anthony Benedicto

Siku moja baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kuzungumzia suala linalomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Mendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, Katibu wa chama hicho, John Mnyika amekosoa baadh ya kauli na kudai kuwa ameingilia uhuru wa Mahakama.

Wakati Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza na chombo cha habari cha BBC Swahili kwa njia ya mahojiano, alipoulizwa kuhusu suala linalomkabili Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe alidai kuwa tuhuma hizo zilianza mwaka jana (2021) Mwezi wa tisa hisipokuwa uchunguzi ulikuwa bado haujakamilika, lakini alieleza kuwa baada ya kukamilisha ndio maana alishikiliwa na Jeshi la Polisi.

“Mbowe alifunguliwa kesi mwezi wa tisa mwaka jana , kwahiyo yeye pamoja na wengine na kama ulivyosema mashitaka ni ugaidi na kuhujumu uchumi nadhani wenzie kesi zao zimesikilizwa wengine wamepewa hukumu zao wanatumikia…Yeye uchunguzi ulikuwa unaendelea, tumeingia kwenye uchaguzi amemaliza uchaguzi sasa hivi polisi wamekamilisha uchunguzi wao wamemuhitaji waendelee na kazi yao” alisema Samia Suluhu Hassan.

Licha ya kulitolea maelezo tofauti jambo hilo lakini mwisho wa maelezo wakati akimjibu mwandishi wa habari wa BBC, Rais Samia Suluhu Hassan aliomba kutolizungumzia suala hilo na kutaka waiachie mahakama ilitolee maamuzi kwa kuwa yeye hana uhuru huo wa kuzungumzia.

“Lakini kwa sababu jambo lipo Mahakamani sina uhuru wa kulizungumzia kwa sana nadhani tuache Mahakama zioneshe Ulimwengu kwamba hizo shutuma wanazomshutumu ni zakweli au sio za kweli, kama za kweli Mahakama itaamua” alisema Rais Samia Suluhu Hassan

Aidha kwa niaba ya Chadema Katibu Mkuu wa Chama hicho aliwaalika waandishi wa habari na kutolea maelezo kauli zilizotolewa na Rais Samia Suluhu wakati akifanya mahojiano kuhusu suala ambalo linamkabili Mwenyekiti wao Freeman Mbowe.

Mnyika amesema kuwa kauli alizozitoa Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu suala la Mbowe ni kuingilia uhuru wa Mahakama na kwamba kauli hizo zinailekeza Mahakama namna kutoa maamuzi ya hukumu, huku akibainisha kuwa kuhusu kauli hizo kuwa tayari Chama hicho kimeshaelekeza mawakili wake kulichukulia hatua jambo hilo.

“Kauli ya Rais SuluhuSamia zina mwelekeo wa kuingilia shauri lililopo mahakamani, zina mwelekeo wa kuingilia uhuru wa Mahakama na zina mwelekeo wa kutoa hukumu kwa kesi. Hivyo tumeshaelekeza mawakili wetu wachukue hatua juu ya kauli hizi” amesema Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika

Aidha kutokana na Rais Samia kwenye mahojiano kujaribu kuhusianisha tuhuma hizo na safari ya nje ya Nchi aliyoifanya Mwenyekiti Freeman Mbowe Miezi michache baada ya kumalizika kwa uchaguzi Mkuu mwaka 2020, kuwa Mbowe alienda Nairobi huku akijua anakabiliwa na tuhuma za jinai, Myika amepinga mtazamo huo na kudai kuwa Mbowe alisafiri kwa kufuata taratibu na hajawai kutafutwa akiwa nje ya Nchi.

“Katika hatua za baadaye tutakuja kueleza kuhusu safari za Mwenyekiti Freeman Mbowe nje ya nchi, ukweli ni kwamba Mwenyekiti Mbowe hakuwahi kutoroka na Mara zote aliposafiri alisafiri kwa taratibu za kisheria na hata alipokuwa nje ya nchi hakuwahi kutafutwa” amesema Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika

Ili kulinda uhuru wa Mahakama ambayo ni muhimili unaojitegemea Nchini Tanzania, sheria na kanuni zimeweka mipaka kwa mtu ya kulizungumzia shauri lililoko Mahakamani ili kutoathiri uhuru wa kufanya maamuzi ya kutoa hukumu, licha hilo lakini pia zipo kanuni ambazo ni katiba zinampa mamlaka Rais ya kuigilia shauri lililoko Mahakamani ambalo alijatolewa hukumu au tayari limeshatolewa hukumu lakini kwa kufuata taratibu maalumu zilizoainishwa.

Pia ikumbukwe kwa sasa ni zaidi ya siku 20 tokea Freeman Mbowe ashikiliwe na kufunguliwa shauri Mahakamani amabalo tayari limeanza kusikilizwa na litaendelea tena Augosti 13, 2021 kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Jijini Dar es Salaam, akikabiliwa na mashitka mawili ya jinai, Kosa la kufadhili Vitendo vya Ugaidi kwa kutoa pesa na kula njama ya kutenda kosa (uhujumu Uchumi).