Katibu wa Halmashauri kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi wa CcM, Shaka Hamdu Shaka amesema kuwa suala la maridhiano sio jipya kwenye Chama chao, amedai kuwa wamekuwa wakifanya majadiliano na upatanishi ndanii na nje ya Nchi, ambapo ameongeza kuwa msingi wa amani katika Nchi ni kusimama pamoja kwa masuala mbalimbali yanayobeba mustakabali wa Taifa
“Katika suala la maridhiano, majadiliano na upatanishi CCM imekuwa ikifanya hayo hapa nchini na hata nje ya nchi, wakati ZAPU na ZANU wanataka kuungana kutengeneza ZANU PF, Mwl. Nyerere alikwenda kushiriki mchakato wa kuwaunganisha” amesema, Shaka
“Hakuna njia nyingine ya kulinda amani, umoja na mshikamano isipokuwa kwa kusimama pamoja na kuwa wamoja kwa masuala yote yanayobeba mustakabali wa taifa letu” Shaka
Ameyasema hayo ikiwa ni siku chache baada ya baadhi viongozi wa ngazi ya juu kataka Chama hicho kukutana na viongozi wa Chadema ngazi ya kitaifa katika kikao cha pamoja na Rais Samia Suluhu Hassan kujadili masuala mbalimbali ya kisiasa.
Habari Zaidi
DCI KINGAI ASISITIZA WAZAZI KUZINGATIA MALEZI BORA KWA WATOTO WAO ILI KUPUNGUZA UKATILI
THRDC,C-SEMA YAENDESHA MAFUNZO KWA POLISI NA WAENDESHA MASHITAKA