February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

CCM KUMCHUKULIA HATUA MBUNGE ALIYEVAMIA MSIBANI

Mbunge Catherine Magige

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeeleza kusikitishwa kwake na  kuchukizwa na kitendo kilichofanywa na mbunge wa viti maalum CCM ,Catherine Magige na baadhi ya viongozi wa UWT mkoa wa Arusha kilichofanyika Mei 27,2021 cha kuingia katika makaburi ya familia  ambako kulikuwa kunafanyika mazishi ya mfanyabiashara Kuzula Madoda ambaye anadaiwa kuwa mchumba wa mbunge huyo.

Katibu wa Itikadi na Uenezi,Shaka Hamdu Shaka amsema chama kinatafakari suala hilo kwa undani kwa mujibu wa Katiba ya chama hicho na kuchunguza tukio hilo ili kuwachukulia hatua za kimaadili wote waliohusika.CCM imeeleza kuchukizwa na kulaani kitendo hicho na kusisitiza kuwa kina imani zaidi katika kujenga uimara wa, kuheshimiana na upendo.

Catherine Magige pamoja na wenzake waliingia makaburini hapo siku ya jana ili kushiriki maziko ya Madoda na watu waliokuwa naye walivunja geti na kuingia ndani ya makaburi ya familia na kuweka shada la maua katika kaburi wakati ibada ya mazishi ikiendelea.Madoda ameacha mke na watoto.

“CCM inaamini katika kujenga uimara wa familia, kuheshimiana ndani ya jamii na kuendeleza upendo katika familia halali, badala ya mivutano na uvurugaji usiokuwa na sababu”Shaka Hamdu Shaka.