February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

C-SEMA YAWAJENGEA UWEZO WASHAURI WA HUDUMA YA SIMU KWA MTOTO KUPITIA NAMBA 116

Mratibu kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Nchini Tanzania Onesmo Olengurumwa hii leo amefungua Mafunzo ya siku tatu yanayolenga kuwajengeaa uwezo washauri wa huduma ya Ulinzi kwa Mtoto ya namba 116 yaliyoandaliwa na shirika Mwanachama wa THRDC, C- Sema na kufanyika katika Ofisi za Mtandao.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mafunzo Hayo, Mratibu ameeleza kuwa “Watoto wanahitaji kulindwa, Watoto ni wadau wakubwa sana katika taifa lolote lile, tusipowalea na kuwaandaa vizuri tunakuwa hatujaliandaa taifa vizuri hivyo ninyi mpo kuhakikisha haki za mtoto zinalindwa na Maslahi ya mtoto yanazingatiwa” Olengurumwa

Huduma ulinzi kwa Mtoto kwa kutumia namba 116 ni huduma isiyokuwa na malipo inayomwezesha mtoto na mwanajamii yoyote kutoa Taarifa pindi vinapotokea vitendo vya ukatili kwa Mtoto kwa saa 24 siku 7 za wiki.