Hatimae mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Wandishi Habari mkoa wa Mbeya,Festo Mwakasege umezikwa kijijini kwao Kilugu,leo Januari 09,baada ya kupatwa na umauti mnamo Januari 07,katika Hospitali ya rufaa ya Mbeya ambako alikuwa akipatiwa matibabu.
Mwakasege ameiongoza Klabu ya Wandishi wa Habari Mbeya,ambayo ilikuwa pia mwanachama wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) tangu mwaka 2019.Mtandao umesikitishwa na kifo cha kiungo muhimu kati yake na Wandishi wa Habari wa mkoa wa Mbeya.
Katika mazishi hayo,THRDC iliwakilishwa na Mratibu wa Mtandao huo Ukanda wa Nyanda za Juu Kusini,ndugu Gabriel John ambae aliwasilisha rambi rambi za mtandao huo kwa niaba ya mratibu wake wa Kitaifa,Onesmo Olengurumwa kwa familia ya Marehemu,ndugu,jamaa,wandishi,pamoja na marafiki.
“Napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru mratibu wa kitaifa Onesmo Olengurumwa, na maafisa wa secretariat ya THRDC, kwa ushirikiano mkubwa walioutoa ikiwa ni pamoja na namna ambavyo wameonesha moyo wa kujali kwa matatizo yanayowakabili wanachama wao, kwani kwenye hili msisitizo ulikuwa mkubwa sana wa kuhakikisha tunashiriki kikamilifu katika mazishi ya mpendwa wetu na mwanachama mwenzetu”,amesema Gabriel John,alipopewa wasaa wa kutoa salamu,kwa niaba ya THRD mara baada ya Mazishi
Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya mpendwa wetu Festo Mwakasege. Amina.
Habari Zaidi
DCI KINGAI ASISITIZA WAZAZI KUZINGATIA MALEZI BORA KWA WATOTO WAO ILI KUPUNGUZA UKATILI
THRDC,C-SEMA YAENDESHA MAFUNZO KWA POLISI NA WAENDESHA MASHITAKA