Kamati ya Huduma ya Maendeleo ya Jamii ya Bunge, imeishauri Serikali izichukulie hatua asasi za kiraia na mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO’s), zinazojihusisha na masuala ya siasa wakati wa uchaguzi, kinyume na misingi ya uanzishwaji wake.
Ushauri huo umetolewa leo Jumatatu na Mbunge Viti Maalum, Mama Salma Kikwete, akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo kuhusu utekelezaji wa majukumu ya bajeti ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, bungeni jijini Dodoma.
“Sheria za uanzishwaji wake zinataka asasi zisizokuwa za Serikali kutojihusisha na siasa, lakini wakati wa kampenzi za uchaguzi kuna baadhi ya asasi zinajipambanua kisiasa na kufanya shughuli za kisiasa jambo ambalo ni kinyume na sheria za nchi,” amesema Mama Salma.
Mama Salma amesema “Kamati inaitaka wizara kuzichukulia hatua asasi zenye mlengo huu na kuzisimamia zijikite katika lengo la kusajiliwa kwake.”
Katika hatua nyingine, Mama Salma amesema kamati hiyo inaishauri Serikali kuzifuta asasi za kiria zisizotekeleza majukumu yake.
Habari Zaidi
DCI KINGAI ASISITIZA WAZAZI KUZINGATIA MALEZI BORA KWA WATOTO WAO ILI KUPUNGUZA UKATILI
THRDC,C-SEMA YAENDESHA MAFUNZO KWA POLISI NA WAENDESHA MASHITAKA