February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

BOTI ILIYOZAMA NIGERIA,WATU 150 HAWAJULIKANI WALIPO

Zaidi ya watu 150 wameripotiwa kutoweka baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kuzama katika mto Niger Kaskazini magharibi mwa Nigeria.

Boti hiyo iliyokuwa imesheheni mizigo na watu ilikuwa likitokea katika jimbo la Niger na kuelekea jimbo la Kebbi na ilizama saa moja tu baada ya kutoka katika eneo inakoegeshwa na mpaka sasa jumla ya watu 20 wamepatikana wakiwa hai na 4 wamefariki dunia huku wengine 156 waliokuwa wameabiri boti hiyo hawajapatikana.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari nchini humo Boti hiyo iliyotengenezwa kwa mbao ni ya zamani na iliyochakaa na ilikuwa imebeba abiria kuliko uwezo wake.

Rais Muhammadu Buhari ametoa salamu za rambi rambi kwa familia namkuielezea aali hiyo kuawa ni ya kutisha