February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

BORIS JOHNSON, BADENI CAMERA ZAWANASA WAKIWA WAMESINZIA MKUTANONI

Pichani, ni picha zilizosambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii Duniani zikiwaonyesha Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson na Rais Joe Biden wa Marekani wakiwa wamesinzia wakati vikao vikiendelea jana jumanne Oktoba 2, 2021 katika Mkutano wa Hali ya Hewa unaofanyika Glasgow huko Scotland

Picha za viongozi hao ambao kutoka kwenye mataifa makubwa zimeibua gumzo na mitazamo mseto katika mitandao ya Kijamii, huku baadhi ya watumiaji wa mitandao wamekosoa hali hiyo lakini wengine wametetea hali hiyo.

Viongozi kutoka nchi zaidi ya 100 duniani akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan wanahudhuria mkutano huo wa 26 unaojadili mabadiliko ya tabianchi, ulioanza Oktoba 31, 2021 na kuendelea hadi tarehe 12 ya mwezi huu wa Novemba mjini Glasgow, Uskochi.