February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

BELARUS : MWANABLOGU ANAYESHIKILIWA ADAIWA KUTESWA AKIWA JELA

Kiongozi wa upinzani wa Belarus, Svetlana Tsikhanovskaya amesema kuwa mwanablogu anayeshikiliwa nchini humo, Roman Protasevich amepigwa na kuteswa akiwa jela.

Wakili aliyemtembelea mwandishi huyo na mpenzi wake, Sofia Sapega alisema yuko salama ila Tsikhanovskaya amewaambia waandishi wa habari kuwa taarifa hiyo ni ya kutiliwa mashaka na ukweli ni kuwa aliteswa na kupigwa.

Kiongozi huyo wa upinzani bado hajatoa ushahidi thabiti kuhusiana na madai yake ingawa familia ya mwandishi huyo katika mkanda wa video imesema mkanda huo ulionyesha dalili za mateso nayaopitia mwanablogu huyo kutoka jela

Protasevich na mpenzi wake walikamatwa mnamo Mei 23 mwaka huu baada ya ndege yao kulazimishwa kutua mjini Minsk.