March 23, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

BARAZA LA KISLAMU, SHURA YA MAIMAMU WAZITAKA MAMLAKA ZA SERIKALI KUWAACHIA VIONGOZI WA CHADEMA

“TAMKO LETU KUFUATIA JESHI LA POLISI NCHINI KUWASHIKILIA VIONGOZI WA CHADEMA

Shura ya Maimamu Tanzania tumefuatilia kwa kina tukio la Jeshi la Polisi kuwakamata viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendrleo CHADEMA. Tumejiridhisha tukio hilo ni ukandamizaji wa Demokrasia na haki za binadamu.

Tumepokea tukio hili kwa masikitiko makubwa.

Kushikiliwa kwa Viongozi hao wa CHADEMA na baadhi ya wanachama hao, kumetokea muda mchache kabla ya kufikia tarehe ya Kongamano la Kikatiba lilio andaliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kufanyika Jijini Mwanza Ukumbi wa Tourist Hotel.

Kukamatwa kwa Viongozi hao ni kiashiria tosha kuwa Jeshi la Polisi nchini lina endeleza hujuma dhidi ya wananchi kwakuwa haki ya kukusanyika na kutoa maoni ni haki ya Kikatiba. Na kuendelea kuwazui Watanzania kutotumia haki yao ni kuvunja Katiba.

Shura ya Maimamu Tanzania inalitaka Jeshi la Polisi Tanzania kuwaachia viongozi wote wa CHADEMA na wanachama wake bila masharti yoyote.

Pia tunazidi kushauri vyombo vya dola ikiwemo Jeshi la Polisi Tanzania, kutoendeleza vitendo vya ukiukwaji haki za raia na kukandamiza uhuru wa watu kujieleza. Kwani vitendo hivi vina leta taswira mbaya kwa taifa letu.”

KATIBU MKUU
Shura ya Maimamu Tanzania