February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

BALOZI WA MAREKANI TANZANIA ATEMBELEA SHIRIKA LA WOTESAWA

Shirika lisilo la kiserikali la WOTESAWA hii Leo tarehe 9/11/2021, wametembelewa na Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Donald J. Wright na Mkewe Kathy Wright, wakiongozana na mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Robert Gabriel, Mganga mkuu wa Mkoa wa Mwanza ndugu Thomas Rutachunzibwa, pamoja na ujumbe wa programu ya Academy for Women Entrepreneurs(AWE) kwa lengo la kuona shughuli zinazofanywa na shirika hilo.

Balozi Wright na mkewe wamefanya mazungumzo na watoto na kuona bidhaa zinazotengenezwa na watoto waliookolewa kutoka kwenye ajira hatarishi ya kazi za nyumbani.