February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

BALOZI WA EU MGENI WA KWANZA THRDC 2022

Na Loveness Muhagazi

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania THRDC, unayo furaha kupata ugeni wa Balozi wa Umoja wa Ulaya Nchini Tanzania, Balozi Manfrendo FANTI.

Balozi FANTI ametembelea mtandao
na kukutana na Mratibu wa Mtandao wa THRDC, Onesmo Olengurumwa, Mratibu wa THRDC- Zanzibar Bw. Abdallah Abeid, Mratibu Msaidizi wa Mtandao THRDC, Bw. Remmy Lema na Kwa Pamoja wamejadili hali ya Watetezi wa Haki za Binadamu Nchini Tanzania pamoja na namna wanaweza kufanya Kazi kwa mashirikiano ya karibu kuhakikisha Watetezi wa Haki za Binadamu wanafanya Kazi katika mazingira salama na wezeshi.

Katika mkutano huo Mratibu THRDC amepata wasaha wa kumkaribisha Balozi FANTI na ujumbe wake katika uzinduzi wa Ofisi za Mtandao zinazotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni visiwani humo lakini pia kutoa nafasi kwa tawi Hilo la Mtandao kushirikiana kwa karibu na ubalozi huo wa Umoja wa Ulaya Ili kuhakikisha Watetezi wa haki za Binadamu visiwani humo wanafanya Kazi katika mazingira mazuri na ya ushirikiano ya Wadau wa maendeleo.

Ikumbukwe Kuwa umoja wa Ulaya hapa Tanzania ndio msimamizi wa mwongozo kwa watetezi wa Haki za Binadamu ulioanzishwa kwa malengo ya kuweka mazingira mazuri ya Watetezi wa Haki za Binadamu ulioidhinishwa na Umoja wa Ulaya mwaka 2004.

TRANSLATION

EU AMBASSADOR PAID A COURTESY VISIT TO THRDC

The Tanzania Human Rights Defenders Coalition THRDC, is pleased to receive a special visit from the European Union Ambassador to Tanzania, Ambassador Manfrendo FANTI who was accompanied by the head of mission Mr. Emilio Rossetti.

Ambassador FANTI visited the Coalition offices and met the THRDC’s Coordinator Mr. Onesmo Olengurumwa, THRDC- Zanzibar’s Coordinator Mr. Abdalla Abeid, Manager of Program, Mr. Remmy Lema and Together have discussed the situation of Human Rights Defenders in Tanzania as well as how they can work in close collaboration to ensure Human Rights Defenders operate in a safe and enabling environment.

During the meeting, the THRDC’s Coordinator welcomed Ambassador FANTI and his delegation to the inauguration of the soon-to-be-launched THRDC Offices in Zanzibar but also to provide an opportunity for the THRDC-Zanzibar branch to work closely with the European Union.

It should be noted that in Tanzania, other countries as well as in multilateral fora, the European Union Delegations’ approach to support Human Rights Defenders is based on the EU Human Rights Defenders Guidelines (firstly approved in 2004), established to support development of conducive environment for Human Rights Defenders, as well as to contribute to reinforcing the EU’s human rights policy in general.