December 4, 2022

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

BABA ALIYEMLAWITI BINTIYE AHUKUMIWA MAISHA, MWANZA

Na Harith Jaha, Mwanza

Mahakama ya wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza imemhukumu kifungo cha maisha mwanaume mmoja Anorld Thomas (30) kwa kosa la kumlawiti mtoto wake wa miaka tisa.

Akisoma hukumu hiyo Hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo Bethseida Sevonike amesema kufuatia ushahidi uliotolewa mahakamani hapo mahakama hiyo imejiridhisha pasipo kuwa na shaka na kumtia hatiani Bw. Thomas mkazi wa Kangae B (Mwanza ) kuwa alitenda makosa hayo kwa nyyakati tofauti vitendo vilivyomuathiri kiafya mtoto huyo wa kike.

Awali wakili wa serikali Martha Mwadenya katika kesi hiyo nambari Mzn/IR/1736/2021 alisema Bwana huyo Thomas alimuingilia kinyume na maumbile mtoto huyo katika mtaa wa Kangae B jijini Mwanza katika nyumba aliyokuwa akiishi na mtoto huyo huku akimtishia kumuua kwa kisu endapo mtoto huyo angewataarifu watu wengine juu ya tukio hilo huku ushahidi wa daktai ukithibitisha kuwa ni kweli mtoto huo aliingiliwa kinyume na maumbile jambo lililomfanya kuanza kuharibika sehemu ya kutolea haja kubwa.

Baada ya hukumu hiyo mama wa mtoto huyo Bi. Suzan Fumbuka amesema ameipokea kwa furaha hukumu hiyo akisema kuwa ilimuumiza kama mzazi anayetamani kumuona binti yake akitimiza ndoto zake huku akiishukuru Watetezi TV kwa ufuatiliaji na ushirikiano wa karibu hadi kuifikia hukumu hiyo.

Anorld alikamatwa tarehe 31 mwezi Machi mwaka huu (2021) ni baada ya kuwekewa mtego uliofanikisha kumnasa na kufikishwa mahakamani ambako hukumu hiyo imetoka.