February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

ASKOFU RUWAICHI: AONGOZA MAZISHI YA PADRI ALIYEKUTWA AMEFARIKI KWENYE TANKI LA MAJI

Askofu  Mkuu Jimbo Katoliki la Dar es salaam ,Yuda  Ruwa’ichi, amesema uchunguzi unaendelea kufuatia kifo cha aliyekuwa Mkuu wa Wamisionari Afrika nchini Tanzania, Padri Francis Kangwa ambaye mwili wake ulikutwa kwenye tanki la maji la nyumba ya mapadri katika jengo la Ottoman,  na kueleza kuwa uchunguzi  utakapokamilika atatoa taarifa.

Askofu Ruwa’ichi amezungumza hayo hii leo wakati akiendesha misa ya mazishi ya Padri Kangwa katika Kituo cha Hija cha Pugu, akiendesha misa ya mazishi ya mwili wa Padri Kangwa na kusema hadi hii leo ambapo mwili wa Padri Kangwa unazikwa hawajapata taarifa kuhusu mazingira ya kifo chake.

“wale mnaododosa kwenye mitandao ya kijamii mtakumbuka kwamba, mwakilishi wa Jeshi la Polisi Dar es Salaam,  alitoa taarifa ambayo ni tamko alituambia uchunguzi unaendelea. Namimi naomba niwaambie  hata leo tunapoenda kumzika Padri Francis hatujapata kauli ya mwisho kuhusu mazingira yote yaliyohusiana na kifo chake,” amesema

“Wamejaribu kututafuta kwa maelezo na wale waliofaulu kunipata niliwaambia kwamba tuanaelewa kilichotokea ni kizito, linafanyiwa kazi na vyombo husika na kwa hiyo kwa wakati huu sina maelezo. Nikiwa na maelezo ya kutoa basi nitawapa,” ameongeza

Aidha Askofu Ruwaichi amewataka watu kukubali kuwa wamepatwa na msiba wenye changamoto na kama wakristo hawana budi kukubali pamoja na kukabiliana nao kama wana wa pasaka na kuwashurkuru wote waliojitokeza katika mazishi ya Padri Francis.