February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

ASKARI 7 WANAODAIWA KUUA MTWARA SASA MAJI YA SHINGO.

lennymapuli@gmail.com

Jeshi la Polisi nchini,limewaomba wakazi wa Mtwara,wenye taarifa za ziada zinazohusu uhalifu mwingine,uliokuwa ukifanywa na Askari 7 wanaodaiwa kumuua mfanyabiashara mmoja mkoani humo,wauwasilishe kwa jeshi hilo,ili kuchukua lichukue hatua zaidi na Haki itendeke.

Msemaji wa Jeshi hilo SACP David Misime,amesema wananchi wapeleke taarifa zozote kwenye timu ya inayochunguza tukio hilo,ambayo mpaka sasa inaendelea kikamilisha uchunguzi wa uhalifu mwingine.

“Yaliyofanywa na askari hawa siyo maelekezo ya polisi,bali ni tamaa tu za kujipatia fedha kinyume na sheria,kanuni,na taratibu za nchi”,inasomeka sehemu ya taarifa iliyotolewa na msemaji wa jeshi hilo.

Mnamo Januari 25,2021,Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Mtwara,ACP Marck Njera,alitoa taarifa kupitia kwa vyombo vya Habari,kuhusiana na mauaji ya kijana mmoja mfanyabiashara wa Madini,Mussa Hamis Musa,yanayodaiwa kufanywa na maafisa 7 wa jeshi la Polisi mkoani humo.Taarifa ya Kamanda huyo wa polisi iliarifu kuwa,tayari jeshi hilo lilikuwa limewatia nguvuni askari wote 7,waliokuwa wakidaiwa kuhusika na tukio lile.