March 23, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

ASHRAF GHANI AKIMBILIA UAE

Rais wa Afghanstan aliyetoroka aliyetoroka nchi yake ,Ashraf Ghani yupo katika nchi ya Umoja wa Falme za kiarabu UAE , Wizara ya mambo ya Nje ya UAE imethibitisha kuwa taifa hilo limefungua milango na kumkaribisha Rais huyo na Familia yake kwa misingi ya kibinadamu.


Ghani alitoroka mji mkuu wa Kabul,Afghanstan siku ya jumapili baada ya wapiganaji wa kundi Taliban walipoukaribia mji huo,amesema sababu kuu yay eye kukimbia ni kuepusha umwagaji wa damu.


Hata hivyo Balozi wa Afghanistan nchini Tajikstan amedai rais Ghani alikuwa amebeba dola milioni 169 wakati alipotoroka nchi yake siku ya jumapili na kueleza kutoroka kwa rais huyo ni usaliti kwa nchi yake.


Kundi la Taliban kwa sasa limetangaza kuchukua utawala nchini Afghanstan baada ya siku ya jumapili kufanikiwa kuudhibiti mji Mkuu wa Kabul, Katika mkutano wa kwanza wa kundi hilo na waandishi wa habari waliapa kulinda haki za wanawake na kusistiza kuwa wanawake wataweza kufanya kazi,kupata elimu chini ya mfumo wa sheria za kiislam.Hadi sasa mataifa kadhaa ya ughaibuni yanaendelea na oparesheni maalum ya kuwaondoa wakimbizi wa Afganstan.