March 23, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

ASAKWA NA POLISI KWA TUHUMA ZA WIZI WA MIFUGO PWANI

Polisi katika Mkoani Pwani  wanamsaka  mfanyabiashara wa nyama (Jina limehifadhiwa) kwa tuhuma za kuchinja mifugo ya wizi na kuuza kwenye mabucha yake binafsi bila kufuata taratibu zozote za ukaguzi wa nyama kwa mujibu wa sheria.

Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Wankyo Nyigesa imesema Jeshi hilo lilipokea taarifa za kupotea kwa  ng’ombe 25  na mbuzi 31 Mali ya Rajabu Maulid  wenye thamani ya zaidi ya Shilingi milion 50 hali iliyowalazimu polisi kuanza msako wa kuwatafuta wahusika wa tukio hilo.

Aidha Kamanda Wankyo amesema  Polisi wamefainikiwa kubaini bucha 7 katika maeneo ya Picha ya Ndege, Kwamathiasi, Loliondo, Kilivya na wakomba ambapo  bucha zote hizo zinadaiwa kumilikiwa na mfanyabiashara mmoja (Anaetafutwa).

“Katika msako tulioufanya tumefanikiwa kukamata kilo 235 za nyama iliyokamatwa na kuteketezwa na wataalamu wa idara ya Mifugo, ng’ombe wanne ambao ni mali ya mtu aitwae Rajabu Maulid” amesema Kamanda Wankyo alipozungumza na wandishi wa Habari.

Vitu vingine vilivyokamatwa ni ngozi za ng’ ombe nane ambao walichinjwa,na mbuzi 24.