March 23, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

ALIYEJARIBU KUMUUA RAIS WA MPITO MALI,AFARIKI

Mwanamume mmoja nchini Mali anayetuhumiwa kwa  kujaribu kumchoma kisu rais wa mpito wa Taifa hilo ,Assimi Goïta juma lililopita amekufa hospitalini akiwa chini ya ulinzi,sababu ya kifo chake inachunguzwa.

Mwanamume huyo, ambaye hajatambuliwa, alikamatwa baada ya kushindwa kutekeleza jaribio hilo la mauaji wakati Goïta alipohudhuria swala msikitini.

Taarifa ya serikali imesema afya ya mtu huyo ilikuwa imezorota akiwa chini ya ulinzi na alipelekwa hospitalini.