Watu watano wamefariki na wengine ambao idadi yao Bado haija fahamika kujeruhiwa baada ya Magari Matatu kugongana usiku wa Juni 21 majira ya saa tano usiku Eneo la Oilcom manispaa ya Morogoro barabara kuu wa Morogoro-Dar es salaam.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi Fotunatus Musilim, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo akisema imehusisha Gari la Abiria Toyota Coster yenye namba za usajiri T686 DUK, Iliyokuwa ikitokea Dar es salaam kuelekea Mbeya , Gari ndogo aina ya Crester yanye namba za usajiri T563 ASA pamoja na Lori la Mizigo kampuni ya Dangote.

“Katika ajali hii,gari aina ya Coaster iliyokuwa inatoka uelekeo wa Dar es Salaam kuja Morogogo lakini ikielekea Mbeya, dereva wa hii gari alitaka kuyapita magari Magari mengine bila kuchukua tahadhali ndio akaenda kuigonga ile Creaster kwa nyuma na kupoteza uelekeo ndipo akaja kugongana uso kwa uso na roli”,amefafanua Kamanda Musilim alipofika eneo la ajali hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa,waliopoteza maisha ni wanaume watatu na wanawake wawili huku akisema majeruhi walipelekwa katika hospitali jirani ikiwemo ile ya rufani Morogoro na taarifa za maendeleo yao zitakuwa zikitolewa kadiri zitakavyotolewa na wataalamu wa afya na kuongeza kuwa waliojeruhi wengi ni waliokuwa wameabiri katika gari aina Coaster.
“Niseme tu kwa kifupi chanzo kikuu cha ajali hii ni uzembe wa dereva wa gari aina ya Coaster aliyetaka kuyapita magari mengine” amesisitiza Kamanda Muslimu na kuwataka madereva kufuata sheria za barabarani,kuzingatia alama na michoro ya barabarani ili kuepusha ajali mbaya ambazo kwa mkoa wa Morogoro zilikuwa zimeanza kupungua.
Habari Zaidi
DCI KINGAI ASISITIZA WAZAZI KUZINGATIA MALEZI BORA KWA WATOTO WAO ILI KUPUNGUZA UKATILI
THRDC,C-SEMA YAENDESHA MAFUNZO KWA POLISI NA WAENDESHA MASHITAKA