February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

AJALI YA BOTI NIGERIA,MIILI 30 YAOPOLEWA

Takribani miili ya watu 30 imeopolewa kutoka katika mto Niger baada ya Boti iliyokuwa na abiria Zaidi ya 180 kuzama siku ya Jumatano.Viongozi wa eneo hilo wanasema mpaka sasa watu 20 wameokolewa wakiwa hai huku wengine hawajulikani walipo.

Inaelezwa kuwa kipindi cha msimu wa mvua, ajali za boti kuzama hutokea mara kwa mara katika mito nchini Nigeria, ambapo baadhi ya boti hupakia abiria wengi kupita uwezo.