February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

AFRIKA KUSINI: WAZIRI ALIYEMCHAPA KIBAO MPORAJI AOMBA RADHI

Kiongozi wa mkoa wa KwaZulu-Natal nchini Afrika Kusini ameomba radhi kwa kumpiga ngumi mmoja wa waporaji wakati akimlazimisha  aweke chini bidhaa alizokuwa ameiba katika bohari moja mjini Durban.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya waziri Mkuu wa Afrika Kusini imesema hatua ya kumkamata mporaji na kumtaka kujisalimisha inakubalika lakini hatua ya kumchap kibao haikubaliki na imesema tayari mwanasiasa huyo ambaye ni Waziri ameomba msamaha kufuatia kitendo hiko.

Tukio hilo lilorekodiwa katika mkanda wa video na kusambazwa katika mitandao ya kijami.Katika vurugu zinazoendelea nchini humo takribani watu 117 wamefariki dunai  na wengine zaidi ya 2,000 wamekamatwa.