February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

AFRIKA KUSINI : JESHI KUTULIZA MAANDAMANO

Afrika Kusini imepeleka majeshi kukabiliana na vurugu zilizoibuka nchinui humo baada ya rais wa zamani wan chi hiyo,Jcob Zuma kufungwa. Katika ghasia hizo zilizoibuka siku ya jumatatu watu takriban sita wameripotiwa kupoteza maisha na wengine 200 wamekamatwa tangu kuanza kwa vurugu hizo.

Zuma mwenye umri wa miaka 79 alikanusha kuhusika katika madai  ya rushwa aliyokuwa akituhumiwa ,alijisalimisha polisi wiki iliyopita ili kuanza  kutumikia kifungo chake cha miezi 15.

Jacob Zuma alihukumiwa kifungo cha miezi 15 jela kwa kosa la kuidharau mahakama baada ya kushindwa kuhudhuria kesi ya madai ya rushwa iliyokuwa ikimkabili.Siku ya Jumatatu  Maduka mbalimbali  yalivamiwa na majengo kadhaa yalichomwa moto wakati wafuasi wake walipoandamana kupinga kifungo hiko.

Jeshi limesema kuwa limeagizwa kusaidia kupunguza ghasia ambazo zimekuwa zikiendelea kwa siku kadhaa.Rais wa Afrika Kusini,Cyril Ramaphosa amesisitiza kuwepo kwa utulivu , akisema hakuna maelezo juu ya vurugu hizo.