Mataifa kadhaa ya ughaibuni yanasema kuna tisho la hali ya juu la kuwepo kwa shambulio la kigaidi katika uwanja wa ndege wa Kabul nchini Afghanstan na kuwaonya raia wao kutosafiri kuelekea huko.
Australia, Marekani na Uingereza tayari zimetoa tahadhari kwa raia wao huku wale waliokuwa nje ya uwanja wa ndege wameshauriwa kuondoka eneo hilo mara moja.
Mpaka sasa ya watu 82,000 wameondolewa Kabul, ambako wanamgambo wa Taliban wamechukua udhibiti wa taifa hilo.Mataifa kadhaa yapo katika harakati za kuwahamisha raia wao pamoja na wakimbizi wa Afghanstan kabla ya Agosti 31,2021.
Kundi la Taliban limekataa kuongezwa muda wa operesheni ya kuwaondoa raia hao na wameahidi kuwaruhusu raia wa taifa hilo na wale wa kigeni kuondoka Afghanstan baada ya tarehe hiyo tajwa.
Habari Zaidi
BULAYA AHOFIA MUSTAKABALI WA WANAHABARI SAMIA AKIONDOKA MADARAKANI
THRDC YAKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA UBALOZI WA JAPAN
THRDC YAWAJENGEA UWEZO WANACHAMA WAPYA WA MTANDAO