
Na: Anthony Rwekaza
Kufuatia kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha ACT Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad, Halmashauri Kuu ya Chama hicho imetangaza rasmi uchaguzi wa kuziba nafasi hiyo.
Kupitia kikao Cha cha Halmashauri Kuu ya Chama cha ACT Wazalendo kilichoketi Oktoba 31, 2021 kilichofanyika Jijini Dar es salaam, zilitangazwa nafasi mbalimbali, ikiwa moja ni ya kiti cha Mwenyekiti na nafasi nyingine ni ya Makamu wa Mwenyekiti Zanzibar na nafasi Mjumbe wa Halmashauri Kuu.
“Halmashauri Kuu ya Chama Taifa ilitangaza rasmi uchaguzi wa nafasi ya Mwenyekiti wa Chama, Makamu Mwenyekiti Zanzibar na Mjumbe wa Halmashauri Kuu. Kwa upande wa Mwenyekiti wa chama, nafasi imetangazwa kufuatia kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Taifa Marehemu Maalim Seif Sharif Hamad aliyefairiki tarehe Februari 17, 2021.” amesema Naibu Katibu wa Habari, Janeth Rithe
Akizungumza na vyombo vya habari kwa niaba ya Chama chake, Naibu Katibu wa Habari Uenezi na Mahusiano na Umma wa ACT Wazalendo, Janeth Rithe amesema kuwa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Zanzibar imetangazwa kufuatia aliyekuwa akiongoza nafisi hiyo, Juma Duni Haji kujiuzuru baada ya kuweka bayana mpango wake wa kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa Chama Taifa.
Pia Janeth Rithe amebainisha siku ambayo chama kupitia mkutano Mkuu kwa mujibu wa Katiba ya Chama hicho wataketi kwa pamoja kumtafuta Mwenyekiti wa Chama Taifa, Makamu Mwenyekiti Zanzibar na Mjumbe wa Halmashauri Kuu, amesema Mkutano huo utafanyika January 29, 2021.
“Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Chama, Makamu Mwenyekiti wa Chama na Mjumbe Mmoja wa Halmashauri Kuu Taifa ambayo nayo ipo wazi, mkutano huo utafanyika kupitia Mkutano Mkuu wa Chama Taifa utakaofanyika Januari, 29, 2021” Naibu Katibu wa Habari, Janeth Rithe
Aidha Amesema Chama hicho kupitia Kamati Kuu ya Chama Taifa kupitia madaraka iliyonayo kikatiba ilifikia hatua ya kuadhimia kuvunja ngome ya Wanawake Taifa ya Chama hicho kwa madai kushindwa kutekeleza majukumu yake, hivyo Chama hicho kilifikia uamuzi kuunda kikosi kazi kinachojumuisha majina matano ambao wate ni Wanawake kwa ajili ya kutekeleza majukumu ya ngome hiyo kwa muda.
Ikumbukwe Chama Cha ACT Wazalendo kiliketi kwa mara ya kwanza kufanya kikao cha Halmashauri Kuu tokea ulipomalizika Uchaguzi Mkuu wa Tanzania uliofanyika October 2021, licha ya hayo yaliyoelezwa pia chama hicho kimetoa maadhimio yaliyotokana na Halmashauri Kuu ambacho ni kikao cha pili katika ngazi ya vikao vya Chama.
Maadhimio hayo pia yamegusia sakata linaloendelea Nchini Tanzania la kuwaamisha wafanyabiashara wadogowadogo maarufu machinga kwenye maeneo ambayo yanadaiwa kuwa sio rasmi, pia wamegusia migogoro ya kisiasa na hali ya amani kwenye mataifa ya Sudan, Ethiopia, Zimbabwe, huku wakiipongeza ngome ya vijana ya Chama hicho kushughulika na sakata la madai ya changamoto mikopo ya elimu ya juu.
Habari Zaidi
KIKOSI KAZI KITASAIDIA KULETA MARIDHIANO – JK
NI MIAKA MITANO SASA TOKEA LISSU ASHAMBULIWE
SHAHIDI JAMHURI AELEZA KINA MBOWE WALIVYOSUKA MPANGO WA KUTENDA UGAIDI