February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

HAKI ELIMU YAADHIMISHA MIAKA 20 TANGU KUANZISHWA

Taasisi ya HakiElimu Nchini Tanzania ambayo ushughulika na masuala ya kukuza elimu, imeadhimisha miaka 20 tokea ilipoanzishwa mnamo mwaka 2001.

Akifungua hafla maadhimisho hayo Mkurugenzi wa taasisi ya HakiElimu Tanzania, John Kalaghe amesema kuwa taasisi hiyo imekuwa ikitoa mchango mkubwa kwenye sekta ya elimu Nchini Tanzania, huku akiishukuru Serikali na wadau kwa ushirikiano wanaoutoa katika kutimiza malengo ya taasisi hiyo.

“Kwa wadau wetu kwa ujumla,wananchi ,walimu ,wanafunzi,marafiki wa elimu,AZAKI,Taasisi za Kifedha na Biashara ,watoa huduma,waandishi wa habari,mmekuwa nguzo pamoja na wafanyakazi mmekuwa wote sehemu ya nguvu kazi kwa kipindi chote cha miaka 20 ya HakiElimu,”John Kalaghe,Mkurugenzi HakiElimu

“kama kuna mchango HakiElimu tunajivunia tumetoa kwa jamii kama kuna mafanikio ambayo tunajivunia kwamba tumetoa katika jamii mafanikio hayo yanawahusu na ninyi pia.Tusingeweza kufanikisha haya yote pasipo msaada wenu,ushirika wenu na pasipo kutuunga mkono,”John Kalaghe,Mkurugenzi HakiElimu.

Pia katika maadhimisho hayo yameenda sambamba na uzinduzi wa kitabu kinachoelezea historia ya HakiElimu Tanzania, pamoja na uzinduzi wa mpango wa maendeleo wa HakiElimu unaotegemewaa kuanza rasmi kutekelezwa mwaka 2022 mpaka 2026.

“Nia na juhudi za pamoja ndio zilizopelekea taasisi ya HakiElimu kuwa na mafanikio.Tunaweza kusema pasipo mchango wenu na hasa wa kitaalamu na kifedha safari hii ingelikuwa na historia nyingine,”John Kalaghe,Mkurugenzi HakiElimu.

“kama kuna mchango HakiElimu tunajivunia tumetoa kwa jamii kama kuna mafanikio ambayo tunajivunia kwamba tumetoa katika jamii mafanikio hayo yanawahusu na ninyi pia.Tusingeweza kufanikisha haya yote pasipo msaada wenu,ushirika wenu na pasipo kutuunga mkono,”John Kalaghe,Mkurugenzi HakiElimu.

“Safari hii ilikuwa na mambo mengi na tusingeweza kufika hapa bila ushirikiano wa serikali,wadau wa maendeleo,marafiki wa elimu ambao ni nguzo kubwa sana ya utekelezaji wa kazi za HakiElimu kule kwenye jamii,wananchi katika sekta mbalimbali na viongozi kwa ujumla walio kwenye maeneo mbalimbali ambayo tunafanya kazi lakini waliopo kwenye sekta ya elimu,”John Kalaghe,Mkurugenzi HakiElimu.

#20YaHakiElimu