Chama cha Waandishi wa Habari wa Kupiga Vita Matumizi ya Dawa za Kulevya na Uhalifu Tanzania (OJADACT ) kimetangaza kupokea taarifa za kutishiwa kwa mwanachama wake Mwandishi Chrictopher Gamaina ikieleza kupokea vitisho toka kwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara Samwel Kiboye kutokana na kuandika habari iliyoonekana kuuchafua uongozi wa Mkoa wa Mara.

Taarifa hiyo ya Mwandishi Christopher Gamaina ilisomeka hivi…
“Leo Mei 19, 2021 saa 9 mchana, Mhariri Mtendaji wa Mara Online News na Sauti ya Mara, Jacob Mugini amepigiwa simu na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Samwel Kiboye maarufu kwa jina la Namba Tatu, akalalamika kwamba leo tumemwandika vibaya kwenye blogu ya Mara Online News (ingawa hakuna sehemu tuliyomtaja kwenye habari anayolalamikia) na kutoa maneno ya vitisho kwa Mugini na mimi Christopher Gamaina – Mhariri Mkuu wa Mara Online News na Sauti ya Mara.
Hivyo naomba msaada wa kukabiliana na vitisho hivyo kwani vinalenga kutuhatarishia maisha na kutuzuia, au kutudhoofisha katika utendaji wetu wa kazi ya kuhabarisha umma.
Wako,
CHRISTOPHER GAMAINA, MWANDISHI WA HABARI
Gamaina”
………………………………………………..

Taasisi ya OJADACT inandelea kulifuatilia tukio kwa ukaribu zaidi ili kupata ukweli na imeiomba Serikali ya Mkoa wa Mara na jeshi la Polisi kufuatilia tukio hilo na kuhakikisha usalama wa waandishi hao.
Habari Zaidi
GENGE LA VIJANA WA KISUKUMA KATAVI LAFUMWA LIKIFANYA “CHAGULAGA”.
AFRICAN COURT ON HUMAN AND PEOPLES’ RIGHTS DELIVERED 14 JUDGMENTS
KESI YA MBOWE:SHAHIDI WA TATU (JAMHURI) AANZA KUTOA USHAHIDI.