February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

Mwanamke mmoja  maarufu Jijini Mwanza aitwaye Swalha, aliyekuwa akijishughulisha na masuala ya urembo (make up artist) aamefariki  dunian kwa kupigwa risasi na mume wake.
Tukio hilo limetokea usiku wa kumkia siku ya  Jumapili ya May 29 2022 nyumbani kwa wanandoa hao huko, Buswelu mkoani Mwanza huku chanzo cha mauaji hayo kikidaiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi.
Taarifa kutoka kwa watu wa karibu zinasema kuwa mume wa Swalha anayejulikana kwa jina la Said alichukua uamuzi huo baada ya
mkewe Swalha kwenda  kuangalia mpira na kuchelewa  kurejea nyumbani. Mumewe hakufurahishwa na kitendo cha mkewe kuchelewa kurudi nyumbani hivyo kukazuka ugomvi baina yao hali iliyopelekea mume wa Swalha kummiminia  risasi mkewe
MAMA SWILHA ALICHOKIELEZA BAADA YA TUKIO
Kuhusu ugomvi kati yao labda ni kuhusu simu, Jumatano iliyopita alipata tenda ya kwenda kumpodoa bibi harusi Shinyanga. Alipofika huko wakati akiwa kwenye kazi mume akawa anapigapiga simu, Swalha akawa anamwambia asimpigie kwa kuwa yupo kwenye kazi.
“Ijumaa jioni akawa anamtafuta hivyohivyo na kumsisitiza arudi nyumbani, Ijumaa hiyohiyo jioni akarudi akafika nyumbani usiku, mume akawa anapiga simu, Swalha akapokea na kumwambia anaomba apumzike kwa kuwa amepodoa watu wengi na amesimama muda mrefu hivyo amechoka.
“Mwanaume akawa anaendelea kupiga simu usiku huohuo, Swalha akalala, alikuja kushtuka saa tisa usiku akakuta miss call 42. Akampigia alivyopokea wakaanza kukwaruzana tena, mwanaume akawa analalamika na kumfokea alikuwa wapi na anafanya nini mpaka hapokei simu.
“Swalha alivyoona wanazidi kugombana akaamua kuweka simu pembeni ili ugomvi usiwe mkubwa.
“Asubuhi yake mume wake akanipigia simu na kusema kuwa mke wake amemjibu vibaya. Kwa hiyo ndio akapanga kurudi Mwanza.
“Baba yake alivyomuita hapa nyumbani nadhani alitaka wazungumze kuhusu hilo, lakini ikatokea wamepishana na mume alivyofika nadhani ugomvi utakuwa uliendelea.
TAARIFA YA JESHI LA POLISI KUHUSU TUKIO HILO
Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ramadhani Ng’anzi ni kuwa ni kweli tukio hilo limetokea kutokana na mgogoro wa ndani wa kifamilia na mtuhumiwa ametoroka, anaendelea kusakwa kwa kuwa alitoroka baada ya tukio.
Kuhusu madai kuwa mtuhumiwa ni mtu wa usalama kama inavyodaiwa na baadhi ya watu amesema sio kweli, ni mvuvi na anamiliki silaha yake kihalali. Jina lake halijatajwa kutokana na sababu maalum.