March 23, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

Chama cha waandishi wa habari wa kupinga vita matumizi ya dawa za kulevya (OJADACT) na uhalifu Tanzania kwa kushirikiana na Taasisi ya Kitaifa ya The Environme tal Reporting Collective (ERC) kimetoa mafunzo ya kuwajengea uelewa wa kuandika habari za uhalifu wa Mazingira Mkoani Mwanza na kuwataka kuandika habari hizo ili kuielimisha jamii.

Mafunzo hayo yametolewa leo April 2 ,2022 Mkoani Mwanza katika ukumbi wa mikutano Nyakahoja kanisani kwa waandishi wa habari 20.
Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana Yonas Alfred aliyezungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo akimuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana amesema kuwa, uhifadhi wa mazingira ni ajenda ya kidunia hivyo amekipongeza Chama hicho (OJADACT) kwa kuendesha mafunzo hayo kwani yatasaidia kuibua uhalifu wa mazingira.
Alfred amesema kuwa bila kutunza mazingira hakutokuwa na viumbe hai akiwemo binadamu kwani kesho haiwezi kukamilika bila kufichua uhalifu wa mazingira.
“Serikali ya awamu ya sita inatoa kipaumbele katika suala la mazingira ndio maana tuna sera ya mazingira na kanuni zinazosisitiza kutunza uhifadhi wa mazingira” amesema Yonas.
Nae Mwenyekiti wa Chama Cha OJADACT Edwin Soko ameongeza kuwa miongoni mwa mazingira ambayo yanatakiwa kuibuliwa ni uhifadhi wa misitu,wanyama na ziwa hivyo mafunzo hayo yatawafanya wawe wabobezi katika kuibua uhalifu wa mazingira hayo.
“Tutumie taaluma zetu kuweza ili kuitunza misitu,wanyama na ziwa Victoria ikiwemo viumbe hai ikiwemo samaki na tuibebe kama ajenda yetu.” alisema Soko.
Kwa upande wa washiriki wa mafunzo hayo ambao ni Hellen Mtereko anaewakilisha chombo cha Fullshangwe amekiomba Chama hicho kuendelea kutoa mafunzo zaidi ili kuielisha jamii ambayo ni walengwa wakubwa huku Deusi Gabone mwandishi wa Kwizera Fm amesema kuwa mafunzo hayo yamemjengea uelewa wa kutosha wa kwenda kuibua uhalifu wa mazingira kutokana na uelewa alionengewa na OJADACT.
Maridhia Ngemela nae ni miongoni mwa waandishi wa habari waliohudhuria mafunzo hayo amesema kutokana na mafunzo hayo na kupata uelewa ambao awali alikuwa hana amesema kuwa ,atajikita zaidi kuandika habari hizo za uhalifu wa mazingira hususani Ziwa Victoria kutoka na kanda ya ziwa kuzungukwa na ziwa ambalo linachangia uchumi wa Nchi.
“Mafunzo niliyoyapata leo yamenipa mwanga wa kujua namna bora ya kuandika habari za mazingira,kwasababu mazingira ndiyo kila kitu katika maisha ya mwanadamu” alisema Maridhia
” nitahakikisha natumia kalamu yangu vizuri ili kuweza kulinda viumbe hai vilivyopo katika ziwa Victoria na vilivyopo ardhini” aliongeza Maridhia.
Mapema mwezi November, 2021 Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alihudhuria Mkutano wa kilele wa mazingira wa Umoja wa mataifa uliofunguliwa huko Glogow nchini Scotland, Uingereza ambao ulizishirikisha nchi 200 duniani.
Akihutubia mkutano huo Rais Samia alitoa wito kwa mataifa yote kuwa juhudi za pamoja zinahitajika kwa kuwa athari za mabadiliko hayo hazichagui nchi zilizoendelea au zinazoendelea.
Itakumbukwa kuwa kwa mapema mwaka huu rais wa Tanzania alikuwa Glasgow kuhudhuria mkutano wa mazingira duniani ambapo aliahidi kuwa Tanzania itashiriki itahakikisha inadhibiti uchafuzi wa mazingira.Kwa mujibu wa UNEP, zaidi ya tani 300 milioni ya uchafu unaotokana na plastiki zinazalishwa duniani kila mwaka.
Kwa sababu plastiki kwa kawaida haziozi kwa haraka, hivyo hazipotei kabisa zinapotua ardhini au majini, bali hubaki na kuendela kuwa ndogo. Tafiti zimeonyesha kuwa, kuna uwepo wa plastiki ndogondogo katika ziwa Victoria, na katika samaki ambao huishi nazo.
Hata hivyo,  habari za uchafuzi unaotokana  na plastiki ndogo ndogo katika nchi za Maziwa Makuu Afrika, haziandikwi kwa wingi ukilinganisha na  nchi nyingine duniani.
Kila mwaka Tanzania imekuwa ikianzisha kampaini mbalimbali za mazingira katika mikoa mbalimbali,yenye lengo la kuhamasisha watu kuendelea kuyahifadhi na kuyalinda maeneo yao bila uharibifu.